Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia nzima ya muziki wa kizazi kipya almaarufu kama Bongo flava Naz D yupo mbioni kurelease video ya nyimbo yake mpya ambayo amehakikisha kuwa  itabamba vilivyo kutokana na style,mashairi na hata mistari iliyotumika kulipika goma hilo linalokwenda kwa jina la Chana Gazeti.Naz D anaongeza kwa kusema: "I'm sure wapenzi wanyimbo za kibongo watafahamu na kuipenda hasa ukiangalia style niliyotumia na aina ya beat yake man!,Nimekuja kitofauti".Kiukweli ni nyimbo ambayo inajaribu kuleta style fulani ambayo wapenzi wengi wanobahatika kutoka viwanja kuruka kopo wamekuwa wakiikosa kwani hakuna asiyejua kuwa zinapopigwa nyimbo za kibongo kopo watu hawajimwagi dancing floor.Aliongeza,Nyimbo za kibongo zimewafanya wapenzi wengi kuzikinai mapema kwani hazichezeki.Sasa kwanini wasanii hamuwapi mashabiki wenu kile ambacho  wanatarajia ? nilimuuliza.Naz D alinijibu kuwa unajua Muziki wa kibongo unaharibiwa na mfumo wetu ulivyokuwa wa uchakachuwaji,Utakuta wasanii wengi wale wanaosikika na kupewa sapoti kubwa ni wale wasiokuwa na uwezo katika taaluma hiyo,ila wapo wasanii wengi walio na vipaji vya kweli hawana wa kuwasaidia au utakuta wanawekewa vigingi kinoma.Mimi nashauri kuwa kama kweli tunataka kuinua mziki wa bongo tuacheni longolongo,madj presenters,wakurugenzi wa vitengo vya burudani,mapromota na waandaaji wa matamasha ya muziki acheni kuangalia tu maslahi ya matumbo yenu pekee wafikirieni na hawa wasanii mnaowapigisha shoo bila malipo stahili,fanyeni haki katika mgawanyo wa haki na sio haki ya mwenye haki itumiwe na mtu asiyetenda haki....,Is not fair, hii sio fair kabisa.Ebwana mimi ni hayo tu ila nawaomba wapenzi mashabiki wa muziki isikilizeni track yangu na mnitumie comments zenu  kupitia facebook page yangu "facebook.com/nasd".Najua kupitia ninyi nitaweza kujua makosa na kujipanga upya nini niwaletee ili niwaburudishe.Chana gazeti inajieleza kwenye track yangu hapo juu,isikilizeni kwanza then tutajulishana malengo ya kutumia title hiyo ya chana gazeti.Nawashukuru sana

No comments:

Post a Comment

Search This Blog