WAKALI MBALIMBALI WALISHIRIKI KUFANIKISHA MPANGO MZIMA!

 Hakuna anayepinga kwamba unapoizungumzia visual lab unamzungumzia Adam Juma, Kiujumla unamzungumzia mtu ambaye kwa hali moja au nyengine amesaidia kutia changamoto katika mabadiliko ya utengenezaji wa video zenye ubora japo kuna challange kubwa kwa wasanii wenyewene juu ya uwezo wao kitaaluma na kisanaa kwa vigezo vya kimataifa.Basi naye alikuwepo kwenye mpango mzima wa kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.Pembeni yake yuko mwanamitindo na mbunifu wa mavazi maarufu nchini Ally Rwemtullah wakipiga pozi za miaka 50.Si unajua hata wasanii wanatakiwa kudizainiwa mavazi ili wawepo kwenye muonekano mzuri???

Bwana eenheeee!!! Hizi pozi sio tu za kuonesha amani yaani kila kitu kipo shwariiii pia pozi zinaoonyesha sura za watu muhimu katika taaluma ya sanaa katika upande wa kucheza na sahani zenye misuguo ya sauti zilizopangiliwa kitaalamu kabisa yaani MASTERING IN DJ SKILLS na Mastyle ya kuchungulia kwa jicho moja lenye uwezo kunata na mapishano ya pixel za camera,bwana jamaa anakwenda kwa jina la DJ Choka, hakuna asiyejua  kwa mikuno yake ya ukweli,along side ni mchizi kwa jina la Dimo Debwe wa Image Profession.Jamaa ni balaa katika eneo zima la kucheza na mistari ya nuendo,Fluity Loop ,Cubes na maprograms mengine mengine kutoa vitu vilivyopikwa yaani mainstrumental ya kweli.Jamaa ukiachana na uwezo wa kuandaa muziki sasa hivi anatisha kwenye fani ya kucheza na camera.Mastill pictures ya ukweli ndani ya hii blog ni kazi yake.Nadhani wadau wengi wanafahamu umuhimu na umakini wa kampuni ya ukweli ya IMAGE PROFESSION kwa Sports &Games,Entertaintment,Visual graphics , film/video production na maeventS kibaooooooo.....
 Wadau wa media walikuwapo kusimamia zoezi zima la Video Make Off.Huyu ni mkurugenzi wa media maarufu nchini katika masuala ya burudani, Clouds TV & FM Radio almaarufu kwa jina la Ruge Mutahaba,akionekana katika pozi la kuridhishwa na mwenendo mzima unavyokwenda sawa.
 Unajua kuna kitu kimoja watu wengi hawajikafaahamu...Kufanya kazi mithili ya kutengeneza filam au video shooting sio tu kumsimamisha msanii na kumcommand "stand by","camera rolling", and "action"...No Noo Noooo!!! Hatuendi hivyo,inafaa apitie steg kadhaa mpaka kufikia hapo.ndio maaana wenzetu wana crew kubwa ya ufanyaji kazi(Make up designer,Costume designer,location manager,production manager na wengine kibao) Nafurahi katika sekta ya kutengeneza video hii hili limezingatiwa.Wakati wa Mapouuwda! wasanii walipigwa make-up kuhakikisha mabaka,makovu au hata vipele havionekani na jicho la camera








No comments:

Post a Comment

Search This Blog