Baada ya miaka mingi kupita huku Tanzania ikiendelea na sifa iliyopewa na Rais mtaafu maarufu kama Mzee Ruksa kuwa ni "Kichwa cha mwandawazimu" akimaanisha ni Taifa linaloshindwa kufanya vizuri katika nyanja hiyo ya michezo mara kwa mara na kuambulia patupu.Hii ilikuwa njia ambayo labda Mzee Ruksa alifikiri ingesaidia kuleta changamoto katika nyanja za michezo na kuwaamsha ili waweze kubuni njia za kuiboost.Lakini cha ajabu kilio chake kiliendelea kupuuziwa, tena kwa mpuuzo wa hali ya juu yaani baada ya wadau na wanamichezo kuchunguza na kutafuta njia mbadala na kama sio kuweka mikakati ya kimaendeleo badala yake tumeshudia wadau hao wakiwemo viongozi wa michezo/wanachama na wengineo wakiwasha moto wa kugombania ruzuku na mafao yanayotokana na misaada ya wafadhili au rambirambi za wanachama huku wakisahau kabisa wajibu walioubeba.Yes! naita rambirambi kwani hata hao wanachama wenyewe wanajidhiki kutoa chochote huku mifukoni wakibakia empty kwa mapenzi ya timu/club zao.Kwa kweli kwa mpenda michezo yoyote lazima atasikitishwana hili kwa kiasi kikubwa sana!!!.Tulishajitahidi kuivaa bendera ya uzalendo mara kadhaa wakati timu zetu zikijitosa kupambana na timu za mataifa mengine lakini tunaambulia kipigo huku tukirudi tukiinamisha vichwa chini.Cha kufurahisha ni hivi karibuni baada ya Bi Sarah kujitokeza na kuandaa mashindano ya Muungano Half Marathon iliyoshirikisha wafukuza upepo wa Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani na baadhi ya wanariadha wa kutoka nchi ya jirani Kenya.Bi Saraha ameeleza kuwa ameamua kuandaa mashindano hayo na ataendelea na azma yake hiyo katika sekta hiyo kwa lengo la kupiga tafu fani hii ya michezo inayoonekana kusahaulika sana katika nchi hii inayosifika na kuwa na watu wengi wenye uwezo wa kuongea na kupanga kuliko kufanyia vitendo ahadi zao.Bi. Saraha anasema lengo analo uwezo anao kauli ambayo ameinukuu kutoka kwa Rais maarufu mstaafu wa Tz Marehemu Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere,Bi Sarah alisema wadau tunahitajika kujitokeza kuinua michezo na tusiache kulaumiana na kuitegea serikali ifanye yote....
No comments:
Post a Comment