Wasanii walipata muda wa kukaa na kuchonga na kutathmini hali halisi ya wao kuitwa kioo cha jamii au kioo cha ......... unaweza kumalizia! kama kinaweza kubadilisha hali ya mfumo mzima wa wao kuvuka boda mpaka mipaka ya wenzetu kuutangaza mziki wa bongo flava na style yetu ya kusheki sijui kiduku au nini? Mimi binafsi sijaijua style inayoitambulisha taifa letu kama ilivyo sauzi na kwaito yao ama Congo na sebene au malewa.
Kazi na dawa, si unajua gari haliendi bila mafuta.Mastar wetu waliweza kuandaliwa msosi wa nguvu,hapa sijui kama kutakuwapo majungu na wale wakusemana wamama- ntilie au wa Kempisky.Chakula cha hadhi ya five star kama hadhi waliyopewa wenyewe.Haya sasa kazi kwenu,sisi ni watazamaji tunatarajia kazi nzuri baada ya video kukamilika tusije tukapeana visingizio kama tuvisikiavyo kutoka kwa wanamichezo wanapofanya vibaya....Msitutunye na nyinyi tukashindwa kutumia muda wetu wa kujiliwaza kwa kusikiliza ama kutizama video za nyimbo zenu badala yake tukabadili chanel kusikiliza wasanii wa nje.Hili linaonekana na linawezekana kama hamtakuwa serious kwa kujua mnachokifanya ni nini.Sasa hivi tumekuwa washabiki wakubwa wa timu kubwa za nje na matamasha ya kitaifa tunaanda kuhimiza support ilhali timu zetu zikiwa taabani,na inawezekana mtu asifahamu hata jina la mchezaji wa timu ya ndani akawafahamu wachezaji watimu nyingi za nje, hii ni mbaya sana...Je na nyinyi mpo tayari kutufikisha huko?????
Kiukweli watu walijipanga kisawasawa kukamilisha mchakato mzima.Kila star alingara ndani ya pamba white iliyodizainiwa kwa nembo ya 50 ikimaanisha 50 year of independent.Hakuna uchakachuwaji japo itifaki nyengine zinaweza kuzingatiwa ila kwa macho yetu ya nje tuna pamba zina quality nzuri tofauti na tunazozoea kuziona.
Huwa nashaangaa sana ninapotazama cinema za Bongo,utakuta mtu mmoja kaplay kazi za kundi la watu ndani ya department kadhaa... yaani mtu mmoja kadirect filam,huyohuyo cameraman na huyohuyo ni editor na anavyeo vingine vingi.Kimsingi lazima kutakuwa na makosa mengi au ulipuaji wa kazi usiozingatia ubora.Hawajui wanashusha CV na P (i.e Personality)zao.Nafurahishwa sana na mpangilio mzima wa mgawanyo wa madaraka uliofanyika katika utengenezaji wa video hii ya miaka 50 ya uhuru.Agalia hapa hawa jamaa tunawaita mastar wapo katika sector ya mapouwda,jamaa wanafanyiwa make up kwa lengo zima la kuifanya video hii ikikamilika camera haitagundua hata kipele au michubuko ya uso....si unajua mambo ya facial scrubbing... Big up crew nzima.This is petraing good imge tuige mazee,hata kama bado upo zama za kiprimittive badilika man!
Hapa sasa ndio kazi inayokusudiwa iko uwanjani.Sina shaka na waandaaji hata crew nzima za uchukuaji picha za mgando na za kutembea.Nimeshaziona kazi zao japo sio kwa kiwango cha kimataifa sana ila wanajitahidi.sisemi wote wapo wengi walipuaji wachache tu tena kwa idadi ndogo ndio waukweli .Hii ni kazi ya wasanii wenyewe sasa tunategemea mapozi na minato ya kwe-enhee kama script yenu inavyoonesha japo sijui level ya vocal iko vipi.Hii ni kazi ya waandaji yaani maproducer ....nachoamini mimi konyagi na sigara kubwa hazina uhusianao wowote na kumbusti msanii kivocal au kiperformance zaidi ya kumharibu na kumuua haraka,hii ni imani kubwa ya wasanii wetu na ndio maana asilimia kubwa ni(@@xxx@@)......sina nia mbaya kusema hivi ni hisia zangu tu! kwa hali moja zinaweza kutubadilisha tukawa level nyengine tukijielimisha na tukaheshimu mipaka na protocal za kazi ama fani tunalizokuwa nazo
Ebwanaaaaa!!!! kweli kazi inaonekana iko seriously.Huyu ni baadhi ya wachukua matukio amboa pozi lake linaonesha kabisa kwamba hayuko tayari kugeuza shingo pembeni akakosa japo tukio moja.Picha hii imechukuliwa na mpiga picha wa Image Profession kuonesha anaheshimu umuhimu wa kushirikiana katika matukio ya msingi.No bifu into dis sector,wat u can c dea iz photography director. He is targeting so as to get cupturing good pictures.Am log out keep ma wordz up one day utanikumbuka!
Mzee wa bongo flava Dully Sykes akijiachia na style yake si unaijua hembu imba kama unaikumka...."chezesha ipinde fanya wainama wainuka ipinde"....haaa inatosha bwana,atleast inachezesha unapata mzuka au unasemaje??
Hawa ni baadhi ya tunaowaita wakali ambao wengine walibahatika kuingia studio kubwa za zombaz nchini marekani japo kuna maneno ya chini ya kapeti hilo sisi hapa halituhusu.Yupo Ali Kiba beneti na Maunda Zorro Huku anayejiita Raisi wa masharobalo na majina kibao si unajua za kibongo vile zilivyo?Hapo ameshikana na mwanadada wa THT Maunda Zoro kwa pamoja wakiwa na mdau muhimu kabisa wa Image profesion na pia mpigaji wa ngoma yaaani producer wa Audio Dimo Debwe ndani ya pozi la kukamata bendera, hii yote kuhashiria mpango mzima wa kuenzi nchi yao inayotimiza miaka 50 ya uhuru inaenda sawa ingawa kuna maswali mengi juu maendeleo kiasi gani tuliopiga kipindi chote hicho......Am not polititian, I get keep ma mouth shut up on this...Alright?
Umeliona hili pozi,hichi ni kikundi cha watu muhimu sana hapa bongo.Kama unataka kutengeneza story utapata novel kutokana na harakati wanazoziendesha kutangaza Kazi zetu kimataifa.Hapa tuna wadau muhimu kama DJ Choka,nani asiyenjua kama jamaa ni hatari katika kusugua sahani zilizojaa signal za sound zenye mpangilio na combination ya ubora.Along side Mzee Dimo ambaye licha ya ukali wa kupanga mistari ya miziki (kuanda miziki) pia jamaa mkali kwenye kucheza na kamera.Hizi picha unazoziona kwenye blog hii ni kazi yake chini ya Image Profession.Nani asiyemfahamu A.Y ni msanii pekee aliyefanya corabolation na wasanii wengi wa nje/ kimataifa kuliko msanii mwengine yeyote Tanzania,hii inahakikisha kuwa jamaa anakubalika sana.Mzee wa nipo bizee...jafarai hazungumziki kwani jamaa ni chata hata kwa watoto...we mpaka maua yanamchanulia.Wazee wa hiphop bange ...walivuma sana kwa uwezo wao wa kutumia kitaa ndani ya rythm za sauto zao zilizopandana kwa mizizimo.Mandnojo na Domo kaya hapa akiwa mmoja kati yao.Yaani kifupi ni shwariiii wewe endelea kufuatilia mengi juu mustakabali wa bongo.Unaruhusiwa kukosoa au kushauri ili tuboreshe,najua sijakamilika hata kalamu hukosea kuandika basi tuma comments zako hata ukiwa umekasirisha kama sio kupendezwa na hisia zangu kwani tukishirikiana tutafika









No comments:
Post a Comment