Naz D aka mzee wa chana gazeti akiwa kwenye pozi ndani ya boti ya abiria.
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia nzima ya muziki wa kizazi kipya almaarufu kama Bongo flava Naz D yupo mbioni kurelease video ya nyimbo yake mpya ambayo amehakikisha kuwa  itabamba vilivyo kutokana na style,mashairi na hata mistari iliyotumika kulipika goma hilo linalokwenda kwa jina la Chana Gazeti.Naz D anaongeza kwa kusema: "I'm sure wapenzi wanyimbo za kibongo watafahamu na kuipenda hasa ukiangalia style niliyotumia na aina ya beat yake man!,Nimekuja kitofauti".Kiukweli ni nyimbo ambayo inajaribu kuleta style fulani ambayo wapenzi wengi wanobahatika kutoka viwanja kuruka kopo wamekuwa wakiikosa kwani hakuna asiyejua kuwa zinapopigwa nyimbo za kibongo kopo watu hawajimwagi dancing floor.Aliongeza,Nyimbo za kibongo zimewafanya wapenzi wengi kuzikinai mapema kwani hazichezeki.Sasa kwanini wasanii hamuwapi mashabiki wenu kile ambacho  wanatarajia ? nilimuuliza.Naz D alinijibu kuwa unajua Muziki wa kibongo unaharibiwa na mfumo wetu ulivyokuwa wa uchakachuwaji,Utakuta wasanii wengi wale wanaosikika na kupewa sapoti kubwa ni wale wasiokuwa na uwezo katika taaluma hiyo,ila wapo wasanii wengi walio na vipaji vya kweli hawana wa kuwasaidia au utakuta wanawekewa vigingi kinoma.Mimi nashauri kuwa kama kweli tunataka kuinua mziki wa bongo tuacheni longolongo,madj presenters,wakurugenzi wa vitengo vya burudani,mapromota na waandaaji wa matamasha ya muziki acheni kuangalia tu maslahi ya matumbo yenu pekee wafikirieni na hawa wasanii mnaowapigisha shoo bila malipo stahili,fanyeni haki katika mgawanyo wa haki na sio haki ya mwenye haki itumiwe na mtu asiyetenda haki....,Is not fair, hii sio fair kabisa.Ebwana mimi ni hayo tu ila nawaomba wapenzi mashabiki wa muziki isikilizeni track yangu na mnitumie comments zenu  kupitia facebook page yangu "facebook.com/nasd".Najua kupitia ninyi nitaweza kujua makosa na kujipanga upya nini niwaletee ili niwaburudishe.Chana gazeti inajieleza kwenye track yangu hapo juu,isikilizeni kwanza then tutajulishana malengo ya kutumia title hiyo ya chana gazeti.Nawashukuru sana

WADAU WASHAURIWA KUJITOKEZA KUAANDA MASHINDANO ILI KUINUA MICHEZO

Baada ya miaka mingi kupita huku Tanzania ikiendelea na sifa iliyopewa na Rais mtaafu maarufu kama Mzee Ruksa kuwa ni "Kichwa cha mwandawazimu" akimaanisha ni Taifa linaloshindwa kufanya vizuri katika nyanja hiyo ya michezo mara kwa mara na kuambulia patupu.Hii ilikuwa njia ambayo labda Mzee Ruksa alifikiri ingesaidia kuleta changamoto katika nyanja za michezo na kuwaamsha ili waweze kubuni njia za kuiboost.Lakini cha ajabu kilio chake kiliendelea kupuuziwa, tena kwa mpuuzo wa hali ya juu yaani baada ya wadau na wanamichezo kuchunguza na kutafuta njia mbadala na kama sio kuweka mikakati ya kimaendeleo badala yake tumeshudia wadau hao wakiwemo viongozi wa michezo/wanachama na wengineo wakiwasha moto wa kugombania ruzuku na mafao yanayotokana na misaada ya wafadhili au rambirambi za wanachama huku wakisahau kabisa wajibu walioubeba.Yes! naita rambirambi kwani hata hao wanachama wenyewe wanajidhiki  kutoa chochote huku mifukoni wakibakia empty kwa mapenzi ya timu/club zao.Kwa kweli kwa mpenda michezo yoyote lazima atasikitishwana hili kwa kiasi kikubwa sana!!!.Tulishajitahidi kuivaa bendera ya uzalendo mara kadhaa wakati timu zetu zikijitosa kupambana na timu za mataifa mengine lakini tunaambulia kipigo huku tukirudi tukiinamisha vichwa chini.Cha kufurahisha ni hivi karibuni baada ya Bi Sarah kujitokeza na kuandaa mashindano ya Muungano Half Marathon iliyoshirikisha wafukuza upepo wa Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani na baadhi ya wanariadha wa kutoka nchi ya jirani Kenya.Bi Saraha ameeleza kuwa  ameamua kuandaa mashindano hayo na ataendelea na azma yake hiyo katika sekta hiyo kwa lengo la kupiga tafu fani hii ya michezo inayoonekana kusahaulika sana katika nchi hii inayosifika na kuwa na watu wengi wenye uwezo wa kuongea na kupanga kuliko kufanyia vitendo ahadi zao.Bi. Saraha anasema lengo analo uwezo anao kauli ambayo ameinukuu kutoka kwa Rais maarufu mstaafu wa Tz Marehemu Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere,Bi Sarah alisema wadau tunahitajika kujitokeza kuinua michezo na tusiache kulaumiana na kuitegea serikali ifanye yote....

MASTAR WA KIBONGO NDANI YA VIDEO MAKE OFF YA MIAKA 50 YA UHURU

 Wasanii walipata muda wa kukaa na kuchonga na kutathmini  hali halisi ya wao kuitwa kioo cha jamii au kioo cha ......... unaweza kumalizia! kama kinaweza kubadilisha hali ya mfumo mzima wa wao kuvuka boda mpaka mipaka ya wenzetu kuutangaza mziki wa bongo flava na style yetu ya kusheki sijui kiduku au nini? Mimi binafsi sijaijua style inayoitambulisha taifa letu kama ilivyo sauzi na kwaito yao ama Congo na sebene au malewa.
 Kazi na dawa, si unajua gari haliendi bila mafuta.Mastar wetu waliweza kuandaliwa msosi wa nguvu,hapa sijui kama kutakuwapo majungu na wale wakusemana wamama- ntilie au wa Kempisky.Chakula cha hadhi ya five star kama hadhi waliyopewa wenyewe.Haya sasa kazi kwenu,sisi ni watazamaji tunatarajia kazi nzuri baada ya video kukamilika tusije tukapeana visingizio kama tuvisikiavyo kutoka kwa wanamichezo wanapofanya vibaya....Msitutunye na nyinyi tukashindwa kutumia muda wetu wa kujiliwaza kwa kusikiliza ama kutizama video za nyimbo zenu badala yake tukabadili chanel kusikiliza wasanii wa nje.Hili linaonekana na linawezekana kama hamtakuwa serious kwa kujua mnachokifanya ni nini.Sasa hivi tumekuwa washabiki wakubwa wa timu kubwa za nje na matamasha ya kitaifa tunaanda kuhimiza support ilhali timu zetu zikiwa taabani,na inawezekana mtu asifahamu hata jina la mchezaji wa timu ya ndani akawafahamu wachezaji watimu nyingi za nje, hii ni mbaya sana...Je na nyinyi mpo tayari kutufikisha huko?????
 Kiukweli watu walijipanga kisawasawa kukamilisha mchakato mzima.Kila star alingara ndani ya pamba white iliyodizainiwa kwa nembo ya 50 ikimaanisha 50 year of independent.Hakuna uchakachuwaji japo itifaki nyengine zinaweza kuzingatiwa ila kwa macho yetu ya nje tuna pamba zina quality nzuri tofauti na tunazozoea kuziona.
 Huwa nashaangaa sana ninapotazama cinema za Bongo,utakuta mtu mmoja kaplay kazi za kundi la watu ndani ya department kadhaa... yaani mtu mmoja kadirect filam,huyohuyo cameraman na huyohuyo ni editor na anavyeo vingine vingi.Kimsingi lazima kutakuwa na makosa mengi au ulipuaji wa kazi usiozingatia ubora.Hawajui wanashusha CV na P (i.e Personality)zao.Nafurahishwa sana na mpangilio mzima wa mgawanyo wa madaraka uliofanyika katika utengenezaji wa video hii ya miaka 50 ya uhuru.Agalia hapa hawa jamaa tunawaita mastar wapo katika sector ya mapouwda,jamaa wanafanyiwa make up kwa lengo zima la kuifanya video hii ikikamilika camera haitagundua hata kipele au michubuko ya uso....si unajua mambo ya facial scrubbing... Big up crew nzima.This is petraing good imge tuige mazee,hata kama bado upo zama za kiprimittive badilika man!
 Hapa sasa ndio kazi inayokusudiwa iko uwanjani.Sina shaka na waandaaji hata crew nzima za uchukuaji picha za mgando na za kutembea.Nimeshaziona kazi zao japo sio kwa kiwango cha kimataifa sana ila wanajitahidi.sisemi wote wapo wengi walipuaji wachache tu tena kwa idadi ndogo ndio waukweli .Hii ni kazi ya wasanii wenyewe sasa tunategemea mapozi na minato ya kwe-enhee kama script yenu inavyoonesha japo sijui level ya vocal iko vipi.Hii ni kazi ya waandaji yaani maproducer ....nachoamini mimi konyagi na sigara kubwa hazina uhusianao wowote na kumbusti msanii kivocal au kiperformance zaidi ya kumharibu na kumuua haraka,hii ni imani kubwa ya wasanii wetu na ndio maana asilimia kubwa ni(@@xxx@@)......sina nia mbaya kusema hivi ni hisia zangu tu! kwa hali moja zinaweza kutubadilisha tukawa level nyengine tukijielimisha na tukaheshimu mipaka na protocal za kazi ama fani tunalizokuwa nazo
 Ebwanaaaaa!!!! kweli kazi inaonekana iko seriously.Huyu ni baadhi ya wachukua matukio amboa pozi lake linaonesha kabisa kwamba hayuko tayari kugeuza shingo pembeni akakosa japo tukio moja.Picha hii imechukuliwa na mpiga picha wa Image Profession kuonesha anaheshimu umuhimu wa kushirikiana katika matukio ya msingi.No bifu into dis sector,wat u can c dea iz photography director. He is targeting so as to get cupturing good pictures.Am log out keep ma wordz up one day utanikumbuka!
 Mzee wa bongo flava Dully Sykes akijiachia na style yake si unaijua hembu imba kama unaikumka...."chezesha ipinde fanya wainama wainuka ipinde"....haaa inatosha bwana,atleast inachezesha unapata mzuka au unasemaje??
 
 Hawa ni baadhi ya tunaowaita wakali ambao wengine walibahatika kuingia studio kubwa za zombaz  nchini marekani japo kuna maneno ya chini ya kapeti hilo sisi hapa halituhusu.Yupo Ali Kiba beneti na Maunda Zorro Huku anayejiita Raisi wa masharobalo na majina kibao si unajua za kibongo vile zilivyo?Hapo ameshikana na mwanadada wa THT Maunda Zoro kwa pamoja wakiwa na mdau muhimu kabisa wa Image profesion na pia mpigaji wa ngoma yaaani producer wa Audio Dimo Debwe ndani ya pozi la kukamata bendera, hii yote kuhashiria mpango mzima wa kuenzi nchi yao inayotimiza miaka 50 ya uhuru inaenda sawa ingawa kuna maswali mengi juu maendeleo kiasi gani tuliopiga kipindi chote hicho......Am not polititian, I get keep ma mouth shut up on this...Alright?
Umeliona hili pozi,hichi ni kikundi cha watu muhimu sana hapa bongo.Kama unataka kutengeneza story  utapata novel kutokana na harakati wanazoziendesha kutangaza Kazi zetu kimataifa.Hapa tuna wadau muhimu kama DJ Choka,nani asiyenjua kama jamaa ni hatari katika kusugua sahani zilizojaa signal za sound zenye mpangilio na combination ya ubora.Along side Mzee Dimo ambaye licha ya ukali wa kupanga mistari ya miziki (kuanda miziki) pia jamaa mkali kwenye kucheza na kamera.Hizi picha unazoziona kwenye blog hii ni kazi yake chini ya Image Profession.Nani asiyemfahamu A.Y ni msanii pekee aliyefanya corabolation na wasanii wengi wa nje/ kimataifa kuliko msanii mwengine yeyote Tanzania,hii inahakikisha kuwa jamaa anakubalika sana.Mzee wa nipo bizee...jafarai hazungumziki kwani jamaa ni chata hata kwa watoto...we mpaka maua yanamchanulia.Wazee wa hiphop bange ...walivuma sana kwa uwezo wao wa kutumia kitaa ndani ya rythm za sauto zao zilizopandana kwa mizizimo.Mandnojo na Domo kaya hapa akiwa mmoja  kati yao.Yaani kifupi ni shwariiii wewe endelea kufuatilia mengi juu mustakabali wa bongo.Unaruhusiwa kukosoa au kushauri ili tuboreshe,najua sijakamilika hata kalamu hukosea kuandika basi tuma comments zako hata ukiwa umekasirisha kama sio kupendezwa na hisia zangu kwani tukishirikiana tutafika

WAKALI MBALIMBALI WALISHIRIKI KUFANIKISHA MPANGO MZIMA!

 Hakuna anayepinga kwamba unapoizungumzia visual lab unamzungumzia Adam Juma, Kiujumla unamzungumzia mtu ambaye kwa hali moja au nyengine amesaidia kutia changamoto katika mabadiliko ya utengenezaji wa video zenye ubora japo kuna challange kubwa kwa wasanii wenyewene juu ya uwezo wao kitaaluma na kisanaa kwa vigezo vya kimataifa.Basi naye alikuwepo kwenye mpango mzima wa kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.Pembeni yake yuko mwanamitindo na mbunifu wa mavazi maarufu nchini Ally Rwemtullah wakipiga pozi za miaka 50.Si unajua hata wasanii wanatakiwa kudizainiwa mavazi ili wawepo kwenye muonekano mzuri???

Bwana eenheeee!!! Hizi pozi sio tu za kuonesha amani yaani kila kitu kipo shwariiii pia pozi zinaoonyesha sura za watu muhimu katika taaluma ya sanaa katika upande wa kucheza na sahani zenye misuguo ya sauti zilizopangiliwa kitaalamu kabisa yaani MASTERING IN DJ SKILLS na Mastyle ya kuchungulia kwa jicho moja lenye uwezo kunata na mapishano ya pixel za camera,bwana jamaa anakwenda kwa jina la DJ Choka, hakuna asiyejua  kwa mikuno yake ya ukweli,along side ni mchizi kwa jina la Dimo Debwe wa Image Profession.Jamaa ni balaa katika eneo zima la kucheza na mistari ya nuendo,Fluity Loop ,Cubes na maprograms mengine mengine kutoa vitu vilivyopikwa yaani mainstrumental ya kweli.Jamaa ukiachana na uwezo wa kuandaa muziki sasa hivi anatisha kwenye fani ya kucheza na camera.Mastill pictures ya ukweli ndani ya hii blog ni kazi yake.Nadhani wadau wengi wanafahamu umuhimu na umakini wa kampuni ya ukweli ya IMAGE PROFESSION kwa Sports &Games,Entertaintment,Visual graphics , film/video production na maeventS kibaooooooo.....
 Wadau wa media walikuwapo kusimamia zoezi zima la Video Make Off.Huyu ni mkurugenzi wa media maarufu nchini katika masuala ya burudani, Clouds TV & FM Radio almaarufu kwa jina la Ruge Mutahaba,akionekana katika pozi la kuridhishwa na mwenendo mzima unavyokwenda sawa.
 Unajua kuna kitu kimoja watu wengi hawajikafaahamu...Kufanya kazi mithili ya kutengeneza filam au video shooting sio tu kumsimamisha msanii na kumcommand "stand by","camera rolling", and "action"...No Noo Noooo!!! Hatuendi hivyo,inafaa apitie steg kadhaa mpaka kufikia hapo.ndio maaana wenzetu wana crew kubwa ya ufanyaji kazi(Make up designer,Costume designer,location manager,production manager na wengine kibao) Nafurahi katika sekta ya kutengeneza video hii hili limezingatiwa.Wakati wa Mapouuwda! wasanii walipigwa make-up kuhakikisha mabaka,makovu au hata vipele havionekani na jicho la camera








USHIRIKI WA MASTAR WA KIBONGO KATIKA MIAKA 50 YA UHURU

Hizi ni miongoni mwa mbwembwe zilizoonesha na baadhi ya wasanii walioshiriki katika harakatiti za utengenezaji wa video ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Search This Blog